Simba na Azam zimeshindwa kufungana baada ya kutoka 0-0 na kuifanya Yanga iendelee kukaa kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara
Mchezo huo ulikuwa muhimu kwa timu zote mbili kutokana na nafasi zao katika ligi
kama Azam ingeshinda mchezo wa leo ingefikisha pointi 61 pointi 4 nyuma ya Yanga lakini kama Simba ingeshinda ingefikisha pointi 60 na kuwa nyuma ya Yanga kwa pointi tano. Matokeo ya leo yanaifanya Yanga kujitanua kileleni kwa kuizidi Azam pointi 6 nyuma ya Yanga huku Simba ikiwa nyuma ya watani zao kwa pointi 7.