Katibu UVCCM Awananga Wapinzani

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wananchi Wilaya ya Same kwenye mkutano wa hadhara.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wananchi Wilaya ya Same kwenye mkutano wa hadhara.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akioneshwa moja ya miradi ya UVCCM wilaya ya Same.

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka akioneshwa moja ya miradi ya UVCCM wilaya ya Same.

Na Woinde Shizza, Same

WABUNGE wa upinzani wametakiwa kuwatetea wananchi, kutatua kero zao pamoja na kuwawakilisha vyema wanapokuwa bungeni na sio kutoka nje ya Bunge hata kwa mambo ya siyokuwa na msingi. Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka wakati akiongea na wananchi wa wilaya ya Same katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kituo cha Mabasi cha Same.

Alisema kuwa ni jambo la kuchekesha na kushangaza kuona kiongozi ambaye amechaguliwa na mwananchi ili akamuwakilishe kwa kupeleka kero zao bunge anafika bungeni na kutoka nje kutokana na sababu zisizo za msingi.

“Unajua ni jambo la kushangaza kuona mbunge anasusia kikao cha bunge kisa eti serekali imekata a kurusha vikao vya bunge ‘live’ sasa jamani uyu mbunge katumwa kuuza sura kwenye televisheni au kupeleka kero za wananchi, mbona awa Wabunge watakuwa kama harusi iliyokosa Vyombo,” alisema shaka.

Alibainisha kuwa wananchi wa nataka kutekelezewa ahadi zao na sio kuona sura zao kwenye tv, na kuaidiwa ahadi zisizo tekelezwa. Alisema kuwa wananchi wa sasa ivi wa nataka maendeleo, na viongozi kuona Sura zao bungeni wakiwa wanafanya mambo ya ajabu na ya kutia aibu wanapokuwa bungeni.

Aliongeza kuwa iwapo kama viongozi wa upinzani wameshidwa kufanya kaziwaliotumwa na wananchi wao basi waachie ngazi kwakijiuzuru ili wanaweza kufanya kazi na wanaotambua nini walichoenda kufanya bungeni wafanyabiashara.

Aidha Alibainisha kuwa viongozi wa Ccm pamoja na serekali wa me jipanga vyema kuhakikisha wanatatua kero za wananchi na kuwaumizia yule yote ambayo wali waaidi wananchi wakati wa kipindi cha kampeni.