Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema ameanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.
Anasema wasiwasi zaidi unatokana na hatari ya klabu hiyo kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika miaka 19.
The Gunners walipoteza nafasi ya kupanda hadi nambari tatu kwenye msimamoli baada ya kutoka sare tasa na Sunderland ugenini Jumapili.
Arsenal, hawajamaliza nne ya nne bora Ligi ya Premia tangu msimu wa 1995-96.
Arsenal ipo pointi tano pekee juu ya Manchester United walio nafasi ya tano, na ambao wana mechi moja hawajacheza