RAIS wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es Salaam amezinduwa rasmi Daraja la Nyerere (Daraja la Kigamboni) linalounganisha Jiji la Dar es Salaam na Mji unaokuwa kwa kasi hivi sasa wa Kigamboni. Daraja hilo ambalo limepewa jina la Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere limeanza kupitika rasmi kuanzia leo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Rais Magufuli amesema kwa sasa wananchi watavuka bure katika daraja hilo hadi pale Serikali itakapotoa mwongozo mwingine. Alisema kwa vyombo vingine kama magari, pikipiki na baiskeli vitavuka kwa tozo kidogo zilizowekwa ili kuchangia gharama za uwekezaji huo uliofanywa kwa ubia na Serikali na Shirika la NSSF.
Kuvunguliwa kwa daraja hilo kubwa na la kisasa kunaleta matumaini mapya kwa wakazi wa Kigamboni ambapo awali walitumia vivuko viwili vya Mv. Magogoni na Mv. Alina ambavyo vilikuwa vikikubwa na changamoto mara kadhaa hasa kutokana na uchakavu na ukarabati wa mitambo ya vyombo hivyo.
Habari zaidi ni hapo baadaye…!