TP Mazembe Wakabiliwa na Kibarua Kigumu

tp-mazembe

klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco katika jitihada zake za kutetea taji lao.

Mazembe wanahitaji kuwafunga Wydad kwa zaidi ya mabao mawili kwa bila ili kunusuru hadhi yao baada ya kuchapwa 2-0 katika mchezo wa kwanza Juma lililopita .

Leo Alex McLeish ataiongoza Zamalek ya Misri kutetea uongozi wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya Mouloudia Bejaia ya Algeria.

Aidha Zesco United ya Zambia inaialika Stade Malien ya Mali. Zesco iko kifua mbele kwa mabao 3-1.

Vile vile mabingwa wa mwaka wa 2014 Entente Setif, ya Algeria waliotoka sare ya 2-2 na Al Merreikh katika mkondo wa kwanza sasa wanawapokea mabingwa hao wa Sudan.