Ratiba ya UEFA Yamkalia Vibaya Manchester City

2353623_UltraWide

Klabu ya Manchester City ya Uingereza imeepuka kukutana na meneja wake wa msimu ujao Pep Guardiola kwenye nusufainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Miamba hao wa Uingereza wamepwa Real Madrid ya Uhispania.
Bayern Munich wa Ujerumani, ambao kwa sasa wamo chini ya Pep Guardiola watakutana na Atlético Madrid ya Uhispania

Droo ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Uefa 2016

Manchester City (Uingereza) v Real Madrid (Uhispania)
Atletico Madrid (Uhispania) v Bayern Munich (Ujerumani)

Mpangilio huo unatoa nafasi ya kuwepo debi ya Madrid fainali iwapo Atletico na Real zitafika fainali au hata kukutanisha Pep Guardiola na klabu yake ya msimu ujao fainali iwapo City na Bayern watafuzu.

Man City watakuwa nyumbani dhidi ya Real Madrid Jumanne 26 Aprili, na ugenini Bernabeu Jumatano 4 Mei.

Atletico Madrid watakutana na Bayern Munich nyumbani Jumatano 27 Aprili na mechi ya marudiano iwe Ujerumani Jumanne tarehe 3 Mei.