Barcelona Yachapwa, Bayern Yanusulika Kutolewa UEFA

1

Klabu ya Barcelona imefungwa na kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 na Atletico Madrid Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid.

2

Atletico Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kufungwa 2-1 Uwanja wa Camp Nou, Barcelona.

Mabao yote Atletico yamefungwa na Antoine Griezmann dakika ya 36 na lingine kwa penalti dakika ya 88

3

Atletico Madrid na Bayern Munich zinaungana na Real Madrid ya Hispania na Manchester City ya England katika Nusu Fainali, ambayo droo yake itapangwa kesho Ijumaa.

A

Bayern Munich imesonga kwa jasho kwenda hatua ya Nusu Fainali baada ya kuitoa Benfica kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 leo Uwanja wa Luz.

BB

Mabao ya Benfica yamefungwa na Raul Alonso Jimenez Rodriguez dakika ya 27 na Anderson Souza Conceicao dakika ya 76, wakati ya Bayern iliyoshnda 1-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani wiki iliyopita, yamefungwa na Arturo Vidal dakika ya 38 na Thomas Muller dakika ya 52.

CC