Yanga Watafuta Rekodi mpya Ligi Kuu Tanzania Bara

yanga

ligi ya kuu Tanzania imeendelea kwa michezo miwili kupigwa kwenye viwanja viwili tofauti, mjini Morogoro kulikuwa na mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Azam FC wakati jijini Dar es Salaam ulichezwa mchezo mwingine kati ya Yanga dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Macho na masikio ya wapenda soka wengi yalikuwa kwenye uwanja wa taifa ambapo mabingwa watetezi wa taji la Vodacom, Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 kwenye mchezo huo uliokuwa mgumu na uliojaa ushindani mwingi.

Yanga walikuwa wakwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Simon Msuva dakika ya tatu kipindi cha kwanza kabla ya Kelvin Sabath kuisawazishia Mwadui FC dakika 10 baadaye Yanga kuandika bao la pili na la ushindi dakika ya 87 likifungwa na Haruna Niyonzima.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Azam FC imeshinda 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
Shukrani kwake, Nahodha John Raphael Bocco aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 62 kwa penalti baada ya mshambuliaji Kipre Herman Tchetche kuchezewa rafu kwenye boksi.

AzamFC sasa inafikisha pointi 55 baada ya kucheza mechi 24, ikiendelea kukaa nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Simba.