Na Janeth Mushi, Arusha
HATMA ya Madiwani watano waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuendelea na uanachama wao au la itajulikana Septemba 20 mwaka huu.
Hatma hiyo itajulikana Septemba 20 baada ya mawakili upande wa
wadaiwa, Method Kimomogolo na wakili upande wa wadai Severine Lawena kuwasilisha pingamizi zao mahakamani hapo kwanjia ya maandishi.
Hawa Mguruta anayesikiliza kesi hiyo alisema anapitia pingamizi za
pande zote mbili na Septemba 20 mwaka huu atatoa uamuzi juu ya hatma ya madiwani hao kama wataendelea kuwa madiwani na kuhudhuria vikao vya Baraza la Madiwani Mkoani Arusha na kupokea posho zao kama kawaida au la.
“Nimepokea pingamizi za pande zote mbili hivyo Septemba 20 nitatoa
maamuzi siku hiyo baada ya kuzipitia kwa makini pingamizi zote mbili
zilizowasilishwa kwa maandishi”. Madiwani hao ni John Bayo, Ruben Ngowi, Rehema Mohamed, Charles Mpanda na Estomii Mallah .
Awali wakili wa utetezi, Method Kimomogolo alidai mahakamani hapo kuwa kwasababu kesi hiyo imefunguliwa kwa dharura hivyo usikilizwaji wake uwe wa dharura.
Kimomogolo katika pingamizi alizota kwa njia ya maandishi zinaeleza
kuwa Mbowe hawezi kushtakiwa binafsi, Chadema haiwezi kushtakiwa kwa jina lake, Maombi ya kufukuzwa uanachama yamepitwa na wakati kwani madiwani hao walishakata rufaa Baraza Kuu la Chama hicho na Mahakama haina uwezo wa kusikiliza ksi hiyo bali Mahakama Kuu ndio yenye uwezo.
Kesi hiyo ya madai yenye namba 17/2011 iliyofunguliwa Agosti 10 mwaka huu na madiwani John Bayo, Ruben Ngowi, Charles Mpanda, Rehema Mohamed na Etomii Mallah ilipinga kufukuzwa uanachama wao na kuomba mahakama kutoa amri ya zuio la muda kwa Chadema kutofanya mikutano ya hadhara na kuwataja majina au kuwadhalilisha kwa namna yoyote ile.
Hakimu Mguruta alidai hawezi kutoa majibu ya pingamizi ya wadai
zilizowasilishwa na mahakamani hapo na wakili Severine Lawena kwani
pingamizi hizo ziliwasilishwa kimaandishi hivyo Septemba 20 ndio
zitasomwa mahakamani hapo.
Hakimu Mguruta awali alitoa siku 14 ili upande wa wadai waweze
kuwasilisha pingamizi zao mahakamani hapo kwani walishindwa
kuziwasilisha kutokana na wakili Lawena kusikiliza kesi nyingine
mahakama Kuu kwa jaji Aisha Nyerere.
Hakimu Mguruta alisema kutokana na Lawena kutofafanua vizuri kwenye
barua yake aliyoiwasilisha mahakamani hapo alitoa muda kwa wakili
huyo upande wa wadai kuwasilisha pingamizi zao kwanjia ya maandishi
Septemba 12 mwaka huu kabla ya saa 7:00mchana na Septemba 20 pingamizi hizo zitajulikana kama zitatupwa ama kusikilizwa.