Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
UONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, umefika Ikulu mjini Zanzibar leo na kumpa mkono wa pole Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spice Islander hivi karibuni.
Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa viongozi hao Makamu Mwenyekiti wa CCM, Tanzania Bara Mhe. Pius Msekwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Mhe.Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai pamoja na viongozi wengine wa CCM, Zanzibar na Tanzania Bara wakiwemo viongozi wa Jumuiya za Chama hicho.
Katika maelezo yake Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM, Tanzania Bara alimpa pole Dk. Shein na kueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi Taifa kimeshtushwa sana na tukio hilo la msiba mkubwa kwa Taifa na kueleza kuwa CCM iko pamoja na viongozi na wananchi wote katika kuomboleza msiba huo.
Mhe. Msekwa alieleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kipo pamoja na wananchi na viongozi katika kipindi hiki kigumu cha msiba na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na moyo wa subira.
Aidha, Mhe. Msekwa alitoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wote wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa mashirikiano mazuri yaliofanywa katika kipindi chote cha msiba pamoja na uokozi.
“Kwa kweli CCM inatoa pongezi wka namna wewe mwenyewe Mhe. Rais ulivyoshirikikikamilifu katika shughuli za uokozi najinsi viongozi nyote mlivyoshughulikia kwa haraka kuanziausiku wa tukio lile hadi hii leo, hongereni sana”,alisema Msekwa.
Pamoja na hayo, alieleza kuwa CCM inapongeza hotuba aliyoitoa Dk. Shein hapo jana mara baada ya dua ya kuwaombea waliofariki katika tukio hilo la kuzama kwa meli, kwani imeweza kueleza namna ya tukio hilo lilivyotokea sanjari na hatua za uogozi zilivyochukuliwa.
Naye Rais Dk. Shein alitoa pongezi kwa ujio wa viongozi hao na kueleza kuwa kwa niaba ya serikali na wananchi wote anachukua nafasi kutoa shukurani kwa uongozi huo kutokana na ujio wao wa kutoa mkono wa pole.
Alisema kuwa tukio hilo ni kubwa na lina majonzi makubwa lakini hata hivyo juhudi kubwa zilichukuliwa na viongozi wa serikali zote mbili, wananchi pamoja na vikosi vya SMZ na vile vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uokozi na kuepekea kupatikana wananchi walio hai na wale waliokufa waliwez kustiriwa kwa kuzikwa.
Dk. Shein aliwaeleza viongozi hao kuwa jitihada za uokozi bado zinaendelea kufanyika na tayari timu ya uokozi kutoka Afrika ya Kusini imewasili kwa lengo la kusaidia katika zoezi la uokozi.
Aidha, Dk. Shein aliueleza ujumbe huo wa viongozi wa CCM kuwaTume ya uchunguzi itakayoundwa inatarajiwa kuwa na wataalamu ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.
Dk. Shein pia, alieleza kuwa maamuzi ya Baraza la Usalama la Taifa yaliotolewa ni lazima yafuatwe kwani yatasaidia kwa kiasi kikubwa na kuwaahidi viongozi hao kuwa jitihada zitafaywa na serikali katika kuhakikisha tukio kama hilo halitokei tena na kuahidi kutoa taarifa kwa wananchi.