MENEJA Mkazi wa Jovago Tanzania, Bw Andrea Guzzoni, amewapongeza Wanzanzibari kwa kitendo cha kudumisha utulivu hata baada ya uchaguzi wa marudio ulofanyika hivi karibuni. Bw Guzzoni alisema kuwa pamoja na kuwa Uchaguzi wa Rais Zanzibar ulifanyika mara mbili lakini bado wananchi wamekuwa watulivu kiasi cha kufanya shughuli za kitalii kutoharibikika kama ilivyotegemewa.
“Zanzibar ni mji wa Utalii, Kama kungekuwa na vurugu za aina yeyote hii ingeharibu shughuli za kiserikali na soko la mji huu kwa kiasi kikubwa”. Aliongezea.
Kwa Upande wake, Lilian Kisasa, Meneja Mawasiliano wa JovagoTanzania, aliongezea kwa kusema kuwa watalii wengi waliokuwa wanaingia Zanzibar na kubook hoteli ni watanzania wenyewe, ambapo idadi ndogo ya watalii kutoka nje ilipungua kwa asilimia 5 tu, Hata hivyo haikuweza kuathiri soko la utalii kwa kiwango kikubwa.
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) iliweza kutangaza marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo yaliyopita kufutwa, ambapo, Dr. Ali Mohamed Shein alitangazwa rasmi kuwa mshindi wa marudio ya uchaguzi wa urais Zanzibar.
Aidha serikali imeombwa kuhimiza hasa utalii wa ndani kwani bado Watanzani wamekuwa wako nyuma katika kutembelea hifadhi zao wenyewe ambapo, hatua hii ikiimarika itaweza kuongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa.