Waziri Mkuu Majaliwa Afungua Mkutano wa ALAT

4

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Akizungumza wakati alipofungua mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016.

1

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Edwin Rutageruka wakati alipotembelea banda la maonyesho la TANTRADE kabla ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kwetu cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016.

2

Wasanii wa kikundi cha Nyota cha Dodoma wakitumbuiza katika Mkutano Mkuu Malum wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma mjini Dodoma Aprili 8,2016.

3

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Jafo kizungumza kabla ya kumakribisha Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kufungua Mkutano Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016.

5

Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016.

6

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT), Gulam Mkadam Taarifa ya Utafiti kuhusu Sekta ya Umma na Binafsi kwenye serikali za Mitaa wakati alipoizindua baada ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa uchaguzi wa Jumuiya ya Tawla za Mitaa Tanzania (ALAT) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Dodoma Aprili 8, 2016. Kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawla za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu