Na, Ferdinand Shayo,Arusha.
Watu wengi wana utamaduni wa kusheherekea siku zao za kuzaliwa maarufu kama Birthday ambapo umri wao umeongezeka hivyo wanajipongeza kwa kufanya tafrija,sherehe,kula na kunywa na hata kufanya kufuru ya pesa na mambo mengine mengi.
Swali la msingi la kujiuliza ni moja tu,umri wako umesonga mbele ,je? nimeacha nini nyuma?
Je? Maisha yako yameacha alama nzuri duniani zisizofutika ambazo ukizitazama unapata ujasiri wa kusonga mbele na kuwa bora zaidi ya jana.
Au unaishi kwa kutimiza idadi ya miaka na kujipongeza pasipokuwa na mchango wowote ule kwa jamii inayokuzunguka.
Ukweli ni kwamba tunaishi duniani ili kutimiza majukumu Fulani na si kutimiza idadi ya miaka ya kuwepo duniani.
Maisha yako yanapimwa na majukumu yako unayoyatekeleza ama mchango wako katika familia,jamii na taifa.
Unapaswa kujipima kuwa katika maisha yako umekua mtu wa kutekeleza majukumu au kutelekeza majukumu.
Hata ukiishi miaka 100 kama huna mchango wowote uliochangia katika jamii yako miaka mingi duniani inaweza isiwe na maana wala tija yoyote jambo ambalo si zuri.
Tafakari juu ya maisha yako una mchango gani katika familia yako,jamii yako na taifa lako na baada yaw ewe kuondoka duniani utakumbukwa kwa lipi ama utasahaulika kirahisi kutokana na kutoacha alama yoyote nzuri ya ukumbusho wako mbali na kuacha watoto au uzao wako.
Hakikisha nyayo zako duniani hazifutiki kwa kuacha alama nzuri isiyofutika kwa kutenda matendo mema na kugusa maisha ya watu wengine kwa kuwasaidia.
Ili hayo yatokee lazima uchukue jukumu zima la maisha yako na kuamua kutimiza wajibu ulionao na si kukwepa wajibu ulionao kwa familia,jamii na taifa kwa sababu usipoyafanya yanayokupasa kuyafanya hakuna atakayefanya na mwisho utaondoka duniani hujafanya lolote na hutakumbukwa kwa lolote pia.
Jambo linguine ni kuacha ubinafsi na kushirikisha wengine zawadi ya vipaji,uwezo tulionao na kuwasaidia wengine kutambua uwezo walionao na kuhutumia kwa faida yao nay a jamii inayowazunguka.
Tafakari utaacha nini kwa kizazi kinachokuja, baada yako tutakukumbuka kwa lipi duniani kwa sababu maisha ya kizazi kijacho yanategemea kizazi cha sasa kilichopo kinatengenezaje mazingira na miundombinu ambayo itatumika na vizazi vijavyo.
Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa “Nusu ya Maisha tunayoishi sasa yanategemea kizazi kilichopita na nusu iliyobaki tunategemea kizazi cha sasa”
Hii ina maanisha kuwa kizazi kijacho kinakutegemea wewe unafanya kitu gani kwa ajili yao na usipofanya hicho kitu hakuna anayefanya isipokua wewe hivyo usipofanya hicho kitu unaacha nafasi iliyo wazi na unaiacha dunia katika ukiwa.
Kizazi kingine kikija kinakuta mashimo au gepu kutokana n na baadhi yaw a watu kutotimiza majukumu yao .
Fikiria teknolojia tunazotumia kompyuta,mifumo ya kibenki ya kielektroniki,waliogundua balbu ,magari ni kizazi kilichopita wengine wameshakufa lakini vitu walivyovigundua na kuvitengeneza vinatumika hadi leo ,fikiri kuwa wasingefanya hivyo dunia ingekua kwenye giza ingekua ukiwa isingekua kijiji kama sasa kwenye utandawazi ama digitali ambayo wameiasisi.
Ni vyema ujue kuwa una nafasi katika hii dunia na dunia inakutegemea na si wewe unaitegemea dunia hivyo ukibadilika utaibadilisha dunia.
UKIBADILIKA UTAIBADILISHA DUNIA
ferdinandshayo@gmail.com
0765938008