Waziri Ummy Mwalimu Akemea Madaktari na Wauguzi Kushambuliwa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wazee aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula mara baada kuwasili hospitalini hapo kuzungumza na wafanyakazi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifurahi jambo na mmoja wa kinamama alipotembelea wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifurahi jambo na mmoja wa kinamama alipotembelea wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikagua neti ya mmoja wa mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikagua neti ya mmoja wa mama aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akemea vikali tabia inayojengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi maeneo mbalimbali.

Waziri Ummy Mwalimu amevitaka vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo hivi ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa kipato cha chini.

Ummy amewasili Mtwara akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi ambapo amefanya mazungumzo na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

Pamoja na hayo waziri huyo amewaonya wananchi kutoitumia vibaya dhamira ya dhati ya Rais Dkt. John Magufuli na Serikali ya kuimarisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa kujichukulia sheria mkononi.