JK ashiriki dua ya kuwaombea waliokufa ajali ya meli Zanzibar

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (watatu kutoka kushoto) akijumuika na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi na wananchi wa Zanzibar katika dua ya pamoja ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya meli iliyotokea mwishoni mwa wiki eneo la Nungwi, Unguja. Viongozi wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Shariff Hamad, kushoto kwa Rais Kikwete ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Picha zote na Freddy Maro wa Ikulu)

Wananchi wa Zanzibar wakiswali wakati wa dua maalumu ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali ya meli ya Spice Islanders iliyotokea mwishoni mwa wiki eneo la Nungwi, Unguja. Swala hiyo ya pamoja ilifanyika leo katika viwanja vya Maisara.

RAIS wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete leo ameshiriki katika dua ya pamoja kuwaombea marehemu waliofariki dunia katika ajali ya Meli ya Mv. Spice Islanders iliyotokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita. Rais Kikwete katika dua hiyo ameungana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi na wananchi wa Zanzibar. Zifuatazo ni picha kuonesha dua ya pamoja.