Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ngazi ya robo fainali imeendelea jana kwa mchezo mmoja, ambapo Mwadui FC wameibuka na ushindi wa mabao 3- 0 dhidi ya wneyeji Geita Gold FC.
Mchezo huo wa kwanza hatua ya robo fainali umechezwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, na Mwadui FC kujipatia magoli yake kupitia kwa Joram Mgeveke, Jeryson Tegete pamoja na Jabir Aziz ‘Stima’.
Baada ya ushindi huo Mwadui FC inasuburi kuungana na timu zingine tatu katika hatua ya Nusu Fainali ambayo michezo yake itachezwa mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kuendelea tarehe 31 Machi kwa michezo miwili, Young Africans watakua wenyeji wa Ndanda FC uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Azam FC wakiwakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo wa mwisho hatua ya nusu fainali utachezwa tarehe 7 April, ambapo Simba SC watakua wenyeji wa Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar ess alaam.
Bingwa wa Kombe la Shirikisho atawakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.