Timu ya Azam FC imefanikiwa kusonga mbele katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika bada ya kuwachapa Bidvest FC kwa jumla ya mabao 7-3
Katika mchezo huo uliopigwa jana jioni katika Uwanja wa Chamazi shujaa wa Azam alikuwa ni mshambuliaji wao Kipre Tchetche aliyefunga mara tatu ‘Hat trick’ akifunga dakika 22,,56 na 88 huku lingine likifungwa na nahodha wake John Boco.
Azam ambayo ilingia katika mchezo huo ikiwa na ushindi wa mabao 3-0 ulioupata ugenini nchini Afrika Kusini kabla ya jana kushinda mabao 4-3 ndiyo waliokuwa wa kwanza kufunga bao likifungwa na Tchetche dakika ya 22 akimalizia kazi safi ya winga Ramadhan Singano ‘Messi’.
Baada ya bao hilo Bidvest waliamka na kuanza kucheza soka la kutafuta bao la kusawzisha lakini wakajikuta wakifungwa bao la pili likifungwa na Bocco aliyepokea mpira wa Tchetche aliyewatoka walinzi wa wageni.
Wageni bada ya bao hilo waliamua kufanya mabadiliko kwa kumtoa Pule Maliele na kuingia Shongwe Jabulani aliyeingia na bahati baada ya kuifungia bao la kwanza timu yake dakika chache kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili Bidvest ambayo iliwachezesha vijana wengi wa kikosi B cha timu yao wakajikuta wakiruhusu bao la tatu likifungwa na Tchetche baad ya kupokea pasi ndefu ya Aboubakar Salum ‘Sure boy’ na Tchetche kumtoka kipa wa wageni Jethren Barr.
Hata hivyo, Bidvest wakatumia makosa ya safu ya ulinzi kupooza kupata bao la pili lililofungwa na Mosiatlhaga Koiekantse dakika ya 58, akimalizia pasi ya Botes Henrico.
Funga nikufunge iliendelea tena dakika ya 88 Tchetche akifunga bao la mwisho la Azam akipokea pasi ya Sure boy kabla ya wageni kufunga bao lao la mwisho dakika ya 90 likifungwa na Botes Henrico kwa kichwa akimalizia krosi ya Lecki Markus.
Kwa matokeo hayo sasa Azam FC takutana na Esperance ya Tunisia katika Raundi ya Pili mwezi ujao.