Wanamichezo na mamilioni ya mashabiki wa michezo kote duniani wanataka majibu kuhusiana na msururu wa kashfa za matumizi ya dawa za kuongeza misuli nguvu iliyoukumba ulimwengu wa michezo
Rais wa Shirika la Kimataifa la Kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza misuli nguvu duniani – WADA Craig Reedie pia ametoa wito kwa wahisani kusaidia kufadhili vita dhidi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni na akaahidi kupewa ulinzi bora wanaofichua siri za uovu huo.
Wakati huo huo, WADA imeipa Kenya hadi Aprili 5 kuthibitisha kuwa inaweza kufanikiwa kulikabili suala la dawa zilizopigwa marufuku, au ifungiwe kushiriki katika michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janiero Brazil.
Sebastian Coe ni rais wa Shirikisho la Kimataifa la Raidah – IAAF na hapa anazungumzia suala hilo huku akizitaja nchi ambazo zinafuatiliwa kwa makini “Kenya, Ukraine na Belarus zimewekwa kwenye orodha ya uchunguzi ya IAAF ya mwaka wa 2016 kuhakikisha kuwa mipango ya kitaifa ya kuapmbana na matumizi a dawa zilizopigwa marufuku michezoni inaimarishwa na hatua za kuitimiza mipango hiyo zinakamilishwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.