Na Dotto Mwaibale
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Masaburi amesema wanachama wa chama hicho waliokiuchumu wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wasitegemee kupata uongozi wowote ndani ya chama hicho.
Masaburi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho na kukipa ushindi ambapo kimeunda Serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.
“Kunawenzetu walitusaliti wakati wa uchaguzi mkuu na kuchangia mkoa wa Dar es Salaam kushindwa kufanya vizuri hali iliyosababisha kuwepo na changamoto hata ya kumpata Meya wenzetu hao tunawafahama na hawatapata nafasi ya kupata nafasi ya uongozi ndani ya chama chetu” alisema Massaburi.
Massaburi alisema ni heri kubakiwa na wanachama wachache waadilifu ndani ya chama kuliko kuwa wengi ambao ni wasaliti na katika jambo hilo ataendelea kulisimamia na kupigania maslahi ya chama ambacho anakitumikia.
Katika hatua nyingine Massaburi aliwataka wana umoja huo kushikamana na kushirikiana na kuhakikisha nguvu yao inaendelea kukipa ushindi chama hicho wa kushika dola kwani jambo hilo linawezekana kwa asilimia 100.