Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Arusha Blandina Nkini amesema kuwa watoto wengi hupata mimba kipindi cha likizo za mashuleni kutokana na ufuatiliaji mdogo wa wazazi kwa watoto wawapo mashuleni na majumbani hali inayochangia ongezeko la mimba za utotoni na kuzorotesha elimu.
Blandina alisema kuwa uzoefu unaonyesha kuwa wazazi wengi hawana muda wa kukaa na watoto wao kuzungumza na wanao juu ya maadili pindi wanaporejea kutoka shule za bweni.
Afisa huyo akizungumza katika mkutano wa kujadili mipango ya mwaka 2016 /17 ya shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation For Tommorrow linalojihusisha na masuala ya watoto ,amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto hasa kipindi ambacho wanakua likizo ili kuwajengea uwezo juu ya changamoto za ukuaji zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hilo Melisa Queyquep amesema kuwa kwa sasa wana mpango wa kutoa mafunzo kwa kwa walimu 500 kwa miaka 5 .
Melisa alisema kuwa wameanzisha mpango huo mahususi ili kuwezesha upatikanaji wa walimu bora kwani vigumu kuwa na elimu bora bila kuwa na walimu bora.
“Kwa sasa tunasomesha watoto 114 wanaosoma kwa ufadhili kwa kipindi cha mwaka huu na pia wanatarajia kuwafikia watoto wengi wa kitanzania ambao ni yatima na wanaishi katika mazingira magumu” Melisa
Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo aliyemaliza muda wake Arusha Kennedy Oulu alisema kuwa serikali inapaswa kuboresha elimu mbali na kujenga majengo pia madawati,vyoo na vifaa vya kufundishia vitiliwe mkazo.