Zlatan Kutimukia Marekani Akifuata Njia za Kina Henry na Beckham

zlatani

Mshambuliaji matata kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic amesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwake kuondoka Paris St-Germain majira ya joto yajayo.

Hii ni baada yake kuwasaidia kutwaa ubingwa mara nne mtawalia Jumapili. Ibrahimovic alifunga mabao manne na kuisaidia PSG kulaza Troyes 9-0 na kutwaa ubingwa wa Ligue 1 zikiwa zimesalia mechi nane.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34 aliambia beIN Sports: “Kwa sasa, sitakuwa PSG msimu ujao. Bado nina mwezi mmoja unusu wa kukaa hapa.

Ibrahimovic amekuwa akihusishwa na kuhamia Manchester United pamoja na Ligi Kuu ya Soka ya Marekani na Canada (MLS).

Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi alisema anataka sana Ibrahimovic asalie baada ya mkataba wake kumalizika Juni.

Ibrahimovic amefunga mabao 27 katika mechi 24 msimu huu na kwa jumla amefunga mabao 102 katika ligi kuu Ufaransa.