Wenger Awashutumu Mashabiki Wanaotaka Aondoke

7

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema mjadala unaotokea kila mara kuhusu hatima yake katika klabu hiyo “umeanza kuwa upuuzi”.

Mfaransa huyo alikuwa akizungumza baada ya Gunners kuondolewa kutoka michuano ya Kombe la FA kwa kuchapwa 2-1 na Watford robofainali.

Arsenal wameshinda mechi moja pekee kati ya saba walizocheza karibuni zaidi.

3

Wenger alisema Mechi inayofuata huwa mtihani tayari na kila mara unageuzwa kuwa mada ya mjadala.

Arsenal watakutana na Barcelona Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kesho Jumatano na wanakabiliwa na mtihani mkubwa ikizingatiwa kwamba walichapwa 2-0 nyumbani.

Alisema Arsenal imeshindwa mechi nyingi kabla na tutashindwa siku zijazo. Lazima tusalie pamoja na kukabiliana na hali na kujiandaa kwa mechi ijayo kwa Imani.