Mkoa Tanga Wapata Kituo Cha Kukuzia Michezo

2

Mkuu wa Mkoa Tanga, Mwantumu Mahiza ameweka jiwe la msingi katika eneo la kituo cha michezo cha kukuzia vipaji lilipo eneo la Mikanjuni jijini Tanga.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi, Mahiza alisema wamejisikia faraja mkoa wa Tanga kupata nafasi hiyo kuwa mkoa wa kwanza kupata kituo cha kukuzia vipaji nchini.

Mahiza alisema uongozi wa Serikali mkoa wa Tanga utashirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA)/TFF katika kusaidia usimamizi wa uendeshaji wa kituo hicho.

Mahiza ameishukuru TFF kwa kuamua kuwekeza katika ujezi wa kituo hicho, ambacho baaade kitatoa nafasi kwa vijana kupata ajira kupitia mpira na shughuli nyingine za maendeleo ya kiuchumi ikiwemo utalii na watu kupata ajira katika kituo hicho.