Salamu za rambirambi toka kwa wasomaji wa mtandao wa dev.kisakuzi.com kuhusiana na ajali ya Meli Zanzibar

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein


Zifuatazo ni salamu mbalimbali za rambirambi na maoni kwa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kutoka kwa wasomaji wa dev.kisakuzi.com na wadau anuai kuhusiana na ajali ya Meli ya Mv. Spice Islander, Zanzibar.
…………………………………………..
*ZUBEIR A. ZUBEIR
Anasema; “Nawapa pole sana wazanziber,msiba ni wetu wote. Allah awafanyie wepesi waliotangulia mbele ya haki,”
……………………………………………
*Edson Elias
Anasema; “Inasikitisha sana kwa tukio lililotokea, kwa kuwa watanzania wote ni ndugu, yatupasa kuwa pamoja katika hili, tuwasaidie wenzetu. Ni masikitiko lakini hatuna jinsi! Munau azilaze roho zao mahali pema peponi!”
…………………………………………..
*Beda S. Msacky
Anasema; “Kwa kweli inasikitisha sana kwa kutokea ajali za mara kwa mara hapa Tanzania. Tunasikitika sana kwa kupoteza ndugu zetu, marafiki zetu, watoto wetu, baba na mama zetu katika ajali za kizembe ambazo zaweza kuepukika. Hasa kinachonipa hasira zaidi ni kwa nini vyombo hivi havikaguliwi mara kwa mara na mamlaka husika? au ndo kusema wameajiriwa kukaa ofisini kwa kupiga soga na kusoma magazeti? Jamani innaniuma sana. Poleni sana wafiwa, Mwenyezi Mungu awatie nguvu na hekma na busara katika kipindi hiki cha majonzi makubwa. Jina la Bwana lihimidiwe.”
……………………………………………
*Samson Msuya
Anasema; “Poleni ndugu zetu wazanzibar tuko pamoja, Mungu awatie nguvu katika tukio hilo.”
…………………………………………….
*EDEN MUNTHALI
Anasema; “Poleni sana majeruhi, na wafiwa wote. Mungu azidi kuwapa faraja.
…………………………………………….
*Godson Matai
Anasema; “Poleni sana ndugu zetu kwa ajali ya basi na ya gari”
……………………………………………
*Abrahman Ali
Anasema; “Tupowe watu wa Zanzibar na Watanzania kiujumla juu ya msiba huu wa kitaifa, poleni wafiwa na hiyo ni kazi ya Allah, Mungu aziweke roho za marehemu pahala pema peponi, Amiin”
……………………………………………
*Mrema Starn
Anasema; “Poleni ndugu zangu. Tupo pamoja”
……………………………………………
*Idrissa Khamis
Anasema; “Ni kweli kwamba ni ajali mbaya sana amboyo imetokea katika bandari yetu lakini bado wananchi wanahamu yakujua ni abiria wangapi ambao walikuemo katika meli hiyo bado kuna utata mkubwa katika familia mbalimbali juu ya ajali hiyo. Tumepata kujua idadi ndogo (250) ya watu ambao wameokolewa lakin bado mamia ya abiria yapo katika kina cha maji. Je ni watu wangapi ambao wameshapoteza maisha yao kiukweli bado hali ni mbaya sana hapa zanziibar kama watu waliookolewa ni hao basi kuna 350 bado wapo katika maafa haya bado tunahitaji msada wa hali ya juu.
…………………………………………….
*Tumaini Sandi
Anasema; “Poleni sana! Kwani inasikitisha.”
…………………………………………….
*Hassan Said
Anasema; “Poleni wafiwa huu ni msiba wa Taifa Mungu tupe uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.”

Hizi ni baadhi baadhi ya salamu za rambirambi na maoni ya wasomaji wetu leo.