Rais Magufuli Apangua Ma RC, Ampa Makonda Dar

Mkuu wa Wilaya (DC) Paul Makonda ambaye anapanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya (DC) Paul Makonda ambaye anapanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko kwa kuwapangua wakuu wa mikoa, kuwahamisha na kuwapandisha baadhi ya Wakuu wa Wilaya kwenda kuwa wakuu wa mikoa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kurugenzi ya mawasiliano ya Ikulu, wakuu wa mikoa walioteuliwa ni pamoja na Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Wakuu wa mikoa wengine walioteuliwa na mikoa yao kwenye mabano ni Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga (Geita), Meja Generali mstaafu Salum Mustafa Kijuu (Kagera), Meja Generali mstaafu Raphael Muhuga (Katavi), Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga (Kigoma), Godfrey Zambi (Lindi), Dk. Steven Kebwe (Morogoro), Kamishna mstaafu wa Polisi, Zerote Steven (Rukwa) na Anna Kilango Malecela (Shinyanga).

Wakuu wa mikoa wengine walioteuliwa na mikoa yao kwenye mabano ni pamoja na Mhandisi Methew Mtigumwe (Singida), Antony Mataka (Simiyu), Aggrey Mwanri (Tabora), Martine Shigela (Tanga), Jordan Mungire Rugimbana (Dodoma), Said Meck Sadick (Kilimanjaro), Magesa Mulongo (Mara), Amos Gabriel Makala (Mbeya), John Vianey Mogella (Mwanza), Daudi Felix Ntibenda (Arusha), Amina Juma Masenza (Iringa), Joel Nkaya Bendera (Manyara), Halima Omary Dendegu (Mtwara), Dk. Rehema Nchimbi (Njombe), Mhandisi Evarist Ndikilo (Pwani), Said Thabit Mwambungu (Ruvuma) na Luteni Chiku Galawa Mkoa Mpya wa Songwe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu wakuu wote walioteuliwa wataapishwa Machi 15, 2016 Ikulu jijini Dar es Salaam.