AJALI iliyohusisha magari matatu imetokea katika barabara ya Mandela eneo la Ally Hamza, Tabata jijini Dar es Salaam, ambapo imesababisha vifo vya watu wanne na kujeruhi wengine 19. Kwa mujibu mwa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema gari ya abiria aina ya DCM ilikuwa inatoka Buguruni ikielekea Ubungo na ilipofika eneo hilo ikiwa kwenye mwendo kasi ghafla ilitokea lori la mchanga likaingia barabarani bila ya taadhari likitokea service road.
Alisema jitihada za dereva wa DCM kusimama ghafla zilishindikana na kujikuta ikipanda kingo za barabara na kuhamia barabara ya magari yanayotokea Ubungo hapo ndipo alipogongana na lori lililokuwa limebeba ng’ombe likiwa nalo kwenye mwendo kasi na madhara hayo.