Serikali Yazishauri Taasisi za Kibenki kuwa na Vilabu vya Michezo

Baadhi ya washindi walifanikiwa kutwaa tuzo hizo za Brazuka Kibenki kutoka benki ya NMB.

Baadhi ya washindi walifanikiwa kutwaa tuzo hizo za Brazuka Kibenki kutoka benki ya NMB.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imezishauri Taasisi za Kibenki zilizopo nchini kuanzisha timu na vilabu vya michezo ili kukuza michezo pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa vijana walio wengi ambao wana vipaji lakini hawana timu za kuwaendeleza.

Hayo yamebainishwa kupitia kwa Waziri mwenye dhamana, Mh. Nape Nnauye mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo tuzo za wachezaji bora walioshinda katika michezo maalum ya BRAZUKA KIBENKI iliyoandaliwa na benki ya Barclays na wadau wengine.

Waziri Nape amebainisha kuwa, Nia ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inakuza michezo na kuwa na fursa za kiuchumi kupitia michezo hivyo taasisi hizo zinazo fursa ya kuongeza ajira na ustawi mzuri wa michezo endapo zitaanzisha timu za michezo na kimashindano kwani zinaweza na zinao wajibu huo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya alieleza kuwa, jumla ya timu 16 zilishiriki huku ikianza 28 Novemba 2015 na kufikia tamati 20 Februari 2016 ilikuwa ni ya aina yake na kutoa mwangaza wa kimaendeleo wa kimichezo ambapo pia imesaidia kuimarisha afya, ushikamano na undugu kwa baina ya wachezaji na washangiliaji ambao wengi wao walitoka katika mabenki shiriki 15 ikiwemo matawi yao ya Tanzania Bara na Visiwani.

Katika tukio hilo, washindi mbalimbali walipatiwa vyeti vya shukrani hii ni pamoja na wadhamini wa mashindano hayo ikiwemo kutoka mabenki, kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) na makampuni mengine walipewa vyeti vya shukrani katika kufanikisha michuano hiyo.

Imeandaliwa na Andrew Chale,ModewjiblogNao

Mwakilishi kutoka MeTL Group, Bw.Zainul Mzige (kulia) akikabidhi cheti cha ushindi kwa Mchezaji Nuhu Mkuchu kutoka benki ya NMB.

nape bora

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akikabidhi tuzo ya golikipa bora, Gabriel Bernard.

Nape boraa

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akikabidhi tuzo ya mfungaji bora mchezaji kutoka benki ya NMB, Ahmed Nassoro.

nape ddf

Baadhi ya washiriki na wageni mbalimbali walifika katika tukio hilo…

nape ff

Mratibu wa michuano hiyo Brazuka Kibenki, Bi. Nasikiwa Berya akikabidhi cheti kwa mmoja wa washindi wa michuano hiyo..

nape na maliz

Rais wa shirikisho la Soka nchini, (TFF), Jamal Malinzi akikabidhi cheti cha ushind kwa moja ya washiriki wa michuano ya Brazuka Kibenki.

nape rr

Baadhi ya washiriki..

nape vbv

Utoaji wa vyeti ukiendelea..

NAPE ZANI

Mwakilishi kutoka MeTL Group, Zainul Mzige akikabidhi cheti kwa mmoja wa washindi wa michuano ya Brazuka Kibenki. Zainul alikabidhi cheti hicho akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ‘MO’.

nape zx

Waziri Nape akimkabidhi cheti Rais wa TFF, Jamali Malinzi, ambapo cheti hicho ni maalum kwa TFF kuongeza mchango wao kaatika kukuza michezo nchini..

Nape112

Waziri Nape akitoa tuzo hizo..

napess

Waziri Nape akitoa tuzo hizo..