Hertha Berlin iko kwenye nfasi nzuri ya kurejea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2000 licha ya kichapo cha kushangaza cha mabao 2-0 na Hamburg
Hertha inayoongozwa na kocha Pal DARDAI iko nyuma ya namba mbili Borussia Dortumund na pengo la pointi 16 na nyuma ya viongozi wa ligi Bayern Munich na tofauti ya pointi 21
lakini inashikilia nafasi ya tatu pointi moja mbele ya Schalke, ambayo itacheza nayo mjini Berlin Ijumaa ijayo.
mwishoni mwa wiki, viongozi Bayern Munich walisalia kileleni na pengo la pointi tano mbele ya mahasimu wao wa karibu katika Bundesliga Dortmund baada ya kutoka sare tasa katika mpambano wao mkali wa der Klassiker.
Licha ya ukosefu wa mabao, kipute hicho kilitimiza matarajio ya wengi kutokana na msisimko ulioshuhudiwa uwanjani kutoka kwa mahasimu hao wawili katika uga wa Dortmund wa Signal Iduna Park ambao ulifurika mashabiki