Na Dotto Mwaibale
JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewaaga Mameja generali, Luteni na Brigedia Generali 16, akiwemo, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Luteni Generali Samwel Ndomba. Tukio la kuwaaga majenerali hao ambao wamestaafu utumisho wao jeshini limefanyika jijini Dar es Salaam leo katika viwanja Twalipo Mgulani saa tatu hadi saa tatu asubuhi ambapo liliambatana na gwaride maalumu la vikosi mbalimbali vya Anga, nchini kavu, majini pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Hafla hiyo ya kuwaaga Magenerali hao iliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Davis Mwamunyange ambapo waaga hao ni wa vyeo mbalimbali vya Brigedia Generali waliokuwa nane, Meja Jenerali sita na Luteni wawili na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali na wastaafu wa jeshi hilo.
Majenerali hao kila mmoja alipata fursa ya kukagua gwaride kila alipowasili viwanjani hapo ambapo kati yao ni Luteni Generali walipata heshima ya pekee na kufanyiwa gwaride lililokuwa tofauti na wengine. Majenerali hao ni Mnadhim Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama JWTZ, Luteni Jenerali Samwel Ndomba ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Mkuu wa Utumishi katika jeshi hilo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wengine ni Mkuu wa Tawi la Usalama na Utambuzi jeshini, Luteni Jeneral Paul Ignas ambaye pia aliwahi kuwa ni Mkuu wa Mjeshi ya kulinda amani Darfur nchini Sudani.
Kwa upande wa Mameja Jenerali ambao walipewa heshima na kukagua vikosi hivyo ni Mkuu wa Jeshi la Nchi kavu, Meja Jenerali Salum Kijuu, Mkuu wa Utumishi Jeshini, Meja Jenerali Vicent Mlitaba, Mkuu wa Jeshi la Anga, Meja Jenerali Joseph Kapwani, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo Duruti mkoani Arusha Meja Jenerali Ezekiel Kiunga.
Wengine ni Mkuu wa Shirika la Mzinga mkoani Morogoro, Meja Jenerali Chalres Mzanila, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Mhunga. Na wengine ambao ni Mabrigedia ni Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Sayansi ya Tiba Lugalo, Brigedia Jenerali Dk.Luhindi Msangi, Mkuu Tawi la Ukaguzi jeshini ambaye pia aliwahi kuwa mkaguzi wa majeshi ya SADC, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga.
Wengine ni Mkuu wa Tawi la Akiba, Brigedia Jenerali Agustino Gailanga ambaye pia aliwahi kuwa mpambe wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Mratibu wa Miradi ya Maendeleo Jeshini, Brigedia Jenerali Mrisho Abdallah, Mkuu wa Kikosi cha Ndege cha usafirishaji, Brigedia Jenerali Ezra Ndimugwango.
Na wengine ni Kamanda wa Brigedi ya Tembo mkoani Songea, Brigedia Jenerali John Chacha, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa jeshini, Brigedia Jenerali Martini Mwankanye na Mkuu wa Shule ya ‘Eflantria’ mkoani Arusha, Brigedia Harodi Mzirai.
Akizungumza mara baada ya hafla hiyo Luteni Jenerali mstaafu Ndumba alifurahia hatua hiyoa na kubainisha kuwa kwa sasa wanaenda kuanza maisha mapya.