Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na watoto wenye ulemavu wa ngozi (albinism) katika ziara yake shule ya Arusha ikiwa ni moja ya kituo alichotembelea mkoani Arusha.
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Arusha wakati wa ziara yake ya kuangalia hali ilivyo katika Vituo, Vyuo na shule zinazolea watoto wenye ulemavu Mkoani Arusha
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na mwanafunzi wa shule ya msingi Themi mwenye tatizo la uoni Bi. Lissa Lucas wakati wa ziara yake shuleni
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Longido mkoani Arusha wakati wa ziara ya kutembelea watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum mkoani hapo juzi Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)