Na; Kiongozigod
Watu watatu wanaodhaniwa kuwa majambazi wameuwawa kwa kupigwa risasi na askari polisi katika eneo la Engosheraton mkoani Arusha.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, naibu Kamishna mwandamizi wa polisi Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema watuhumiwa hao wameuwawa wakati wa majibishano ya risasi na askari polisi waliokuwa nyumbani kwa wahalifu hao.
Mnamo tar.27/2/2016 majira ya asubuhi jeshi la polisi jijini hapa walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa eneo hilo la Engosheraton Sinon kuna kijana mmoja wanamtilia shaka kuwa anajihusisha na matukio ya uhalifu.
Amesema jeshi la polisi liliweka mtego na kufanikiwa kumkamata Athumani Ramadhani na alipopekuliwa alikutwa na milipuko ya aina ya TMV6 WATER EXPLOSIVE 17 GIOGEL KUBELA 10,makoti makubwa 2 pamoja na kofia moja ya kuficha uso(mask) na baada ya kumfanyia mahojiano aliwaambia wenzake wawili wanaoshirikiana.
Kamanda Sabas amesema walipofika eneo walilopo wenzake alipiga kelele na wakaanza kushambuliana na jeshi la polisi hivyo mpaka kufikia hatma ya kuwashinda kwa kuwapiga risasi.
“Upekuzi ulipofanyika katika chumba chao hao wahalifu wawili walikuta vitu vifuatavyo Sare 5 za JWTZ(COMBAT),bunduki aina ya AK 47 ikiwa na risasi 18, pikipiki moja iliyobomolewa yenye namba bandia MC 983 BMK,Bendera 2 nyeusi zenye maandishi ya kiarabu zinazotumiwa na makundi ya kigaidi pamoja na Kisanduku cha chuma”amesema kamanda Sabas.
Hata hivyo kamanda Sabas amesema miili ya marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Maunt Meru kwa ajili ya utambuzi wa ndugu na jamaa zao wa karibu.