TPB Yatoa Mikopo kwa Vikundi vya SACCOS Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya akimpa mfano wa hundi wenye thamani ya shilingi milioni 100 kwa Saccos ya TWCC Kigoma, aliyepokea ni Mwenyekiti wa Saccos hiyo Dorothy Takwa. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akishuhudia makabidhiano hayo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akiongea na wana-saccos kabla ya kuwakabidhi kiasi cha fedha Shs milioni 175/= Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi. Beng’ Issa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya

Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Posta Tanzania, Henry Bwogi akimpa zawadi mmoja wa mwanachama wa Saccos, kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki Tanzania, Timotheo Mwakifulefule.

Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Posta Tanzania, Henry Bwogi akimpa zawadi mmoja wa mwanachama wa Saccos, kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Benki Tanzania, Timotheo Mwakifulefule.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya akimpa mfano wa hundi wenye thamani ya shilingi milioni 75 kwa Saccos ya Ishimwe Kigoma, aliyepokea ni  Kaimu Mwenyekiti wa Saccos hiyo Gabriela Hangula. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akifurahi wakati wa makabidhiano hayo.

KATIKA jitihada za kuwafikia Watanzania wengi zaidi na kuwawezesha kiuchumi,Benki ya Posta Tanzania (TPB) imekabidhi mikopo kwa vikundi viwili vya SACCOS ambavyo ni TWCC Women SACCOS na Ishimwe Saccos Mkoani Kigoma. Mikopo hiyo miwili yenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 175 (milioni Mia Moja Sabini na Tano) , itawafaidisha vikundi vyenye jumla ya wanachama takribani 40 chini ya udhamini wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania (NEEC).
Makabidhiano hayo yalifanywa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki Posta, Sabasaba Moshingi na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Bi. Beng’ Issa, kwenye ofisi za Benki ya Posta tawi la Kigoma. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema, “Leo tunashuhudia utekelezaji wa makubaliano yetu ambapo vikundi Viwili vya SACCOS vitapatiwa mikopo yenye masharti nafuu kwa makubaliano maalumu na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania.
Mikopo hiyo yenye jumla ya Shilingi 175,000,000 (milioni Mia Moja Sabini na Tano tu), ambayo itawanufaisha wajasiriamali wana-saccos 40. “Napenda kutoa rai kwa wanajasiriamali wengine nchini kote, wajiunge kwenye vikundi ili waweze kufaidika na mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na benki yetu. Tunaamini kuwa mikopo hii itawasaidia sana kuinua vipato vyenu kwa kukuza mitaji, aliongeza Moshingi.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania Beng’i Issa alitoa pongezi kwa Benki ya Posta Tanzania kwa kushirikiana nao katika kuwawezesha wajasiriamali mbalimbali kwenye changamoto za kujikwamua Kiuchumi.
“Makubaliano tuliyosaini kati ya Benki ya Posta na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania ni moja ya michango muhimu katika kukabiliana na tatizo hili kubwa la ajira nchini, pia napenda kuwaahasa, wanavikundi mliopata mikopo leo hii, mchukue fursa hii kuitumia mikopo yenu vyema na kujenga uaminifu uliomo baina yenu na Benki”, aliongeza Beng’i Issa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya aliwashukuru kwa pamoja Benki ya Posta na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Uchumi Tanzania kwa kuwasaidia wakazi wa Kigoma, pia aliwaomba wana-saccos hao ambao wanapata mikopo hiyo kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa. “Baadhi ya wanachama siyo waaminifu kwani hushindwa kurudisha fedha walizokopeshwa kwa ajili ya kuendeshea miradi yao, hali inayokwamisha wanachama wengine wasipate mikopo kwa wakati,” alisema Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.
Benki ya Posta Tanzania ni miongoni mwa mabenki yanayokuwa kwa kasi nchini, ikifuata sera ya financial inclusion, yaani kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za kifedha hapa nchini.