|
Wafanyakazi wa Tigo wakisaidia kushusha mabati yaliyotolewa na Tigo ikiwa pamoja na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi, mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana
Iringa, Februari 17, 2016:
Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika wodi za Pawaga na Idodi, iliyosababisha watu wengi kukosa sehemu za kulala, mkoani Iringa. Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa mafuriko na
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kusini Jackson Kiswaga, aliesisitiza ahadi ya kampuni kusimama kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida. “Tupo hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa
pole walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema Kiswaga Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni mabati 350, magodoro 30 na
mashuka 35. Mvua zilizonyesha katika wodi hizo, iliripotiwa kwamba
zilisababisha watu 1,155 kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya watu yaliharibika au kubebwa na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Iringa mhe.Amina Masenza. Msaada kutoka Tigo, kulingana na Kiswaga, ni katika mpango
wake wa uwajibikaji kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza baadhi ya rasilimali za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika kusaidia jamii majanga yanapo ibuka.
|