Ushabiki Wamghalimu Mchezaji wa Lokomotiv Moscow

ur2

Mchezaji wa Lokomotiv Moscow anaitwa Dmitri Tarasov anaweza kupewa adhabu na UEFA kutokana na kuvaa T shirt ambayo ina maandishi ya ki-russia yenye maana ya “The Most Polite President” na picha ya Putin akiwa na mavazi ya kijeshi.
ur3

Dmitri alifanya hivyo kwenye mechi dhidi ya Fenerbahce huko Uturuki. Uhusiano wa Russia na Uturuki sio mzuri kutokana na Uturuki kutungua ndege ya Russia mwaka jana ilivyoingia kwenye mpaka wa Uturuki bila utaratibu maalum.

uru1

hivyo kuonyesha t shirt hiyo hapo uwanjani inaweza kuashiria ugomvi kati ya mashabiki wa club hizo mbili ambapo moja ni ya Uturuki na nyingine ya Russia.

Kwa taratibu za UEFA haziruhusu mechi zake na wahusika wa mechi kujihusisha kwa njia yoyote na mambo ya siasa kama alivyofanya Dmitri.