Inasemekana kwamba Chelsea hawajapata kipigo cha magoli 2-1 pekee yake bali walikutana na gesi ya kutoa machozi pale pale ndani ya uwanja. Kwenye mechi ambayo imechezwa kwenye uwanja wa Parc Des Princes kati ya PSG Vs Chelsea askari wa France walitumia mabomu ya machozi kwa mwaka wa pili mfululizo Chelsea wanavyocheza uwanjani hapo.
Kuna mashabiki ilibidi waondoke kipindi cha kwanza hata kabla Mikel Obi hajafunga goli la kusawazisha kutokana na moshi uliotokana na kupulizwa kwa gesi hiyo hapo uwanjani.
Sababu kubwa ya kupulizwa hiyo gesi ni kwa ajili ya kutuliza fujo lakini askari mmoja alisema imepulizwa kwa bahati mbaya kwasababu hakukua na fujo yoyote iliyohitaji kupulizwa hiyo gesi hapo uwanjani.
Lakini baada ya Mikel Obi kufunga goli la kusawazisha na ushangiliji kuendelea kwa kasi muda wa mapumziko, kukatoea tishio la kupulizwa tena gesi hiyo kutoka kwa askari waliokuwepo hapo uwanjani.
Pia kulikua na fujo nyingi nje ya uwanja ambazo zilisababishwa na mashabiki wa Chelsea. Mfano kuna video imerekodiwa ikiwaonyesha mashabiki wa Chelsea wakimzuia mtu mmoja kuingia kwenye treni. Hapo walikua na hasira zao baada ya mechi ya kuisha kwa 2-1.