Katibu Rwegasira Atembelea Ofisi Za Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro

1

Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, John Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani humo.

2

Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, John Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani humo.

3

Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) azungumze na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Rwegasira aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.

4

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) akizungumza na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Meja Jenerali Rwegasira katika hotuba yake aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.

PIX 5

Kaimu Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Holili, Edwin Mwasota akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (watatu kulia) moja ya ofisi zilizopo katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Meja Jenerali Rwegasira alifanya ziara ya kikazi kwa kutembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani Kilimanjaro.

6

Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kushoto) akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto) mpaka Tanzania pamoja na Jengo la Uhamiaji la nchini Kenya (Taveta) wakati walipokuwa juu ya ghorofa ya Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro.

7

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) akiondoka katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumaliza ziara yake ya kulitembelea jengo hilo na kuzungumza na maafisa mbalimbali wa serikali wanaotoa huduma za mpakani mkoani humo. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku na Kulia ni Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpakani Holili, Aden Mwakalobo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi