Dk. Bilal awapa changamoto Magavana Afrika

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akifungua mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Afrika (ACBF) jana mjini Arusha (Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO-Arusha)

Na Janeth Mushi, Arusha

NCHI za Afrika zimetakiwa kuziwezesha mamlaka za kitaifa ili ziweze
kutoa huduma muhimu kwa jamii kwa kukusanya kodi na matumizi bora ya mapato. Changamoto hiyo imetolewa leo na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal wakati akifungua mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo katika Bara la Afrika (ACBF) unaofanyika jijini hapa.

Alisema moja ya eneo muhimu linalotakiwa kuchukuliwa na taasisi hiyo
ni kuimarisha ukusanyaji wa rasilimali za ndani ya Bara la Afrika.
Alisema Afrika inatakwia kuimarisha uwezo wa ukusanyaji na utunzaji wa
rasilimali zake za ndani ikiwa ni kusaidia mamlaka za kitaifa kutoa huduma muhimu kwa jamii kama vile sekta ya elimu.

“Ni muhimu kuwa na uongozi imara katika kusimamia raslimali ili kuweza
kwamba nchi zinatumia raslimali hizo kikamilifu,” alisema Bilal. Alisema kuwa nchi ili iweze kwua namafanikio inahitaji kuwa na uwezo wa kufahamu umuhimu wa taasisi zilizopo nchini mwao ili kushirikiana anazo katika kutatua matatizo hali itakayowezesha taasisi zisijinufaishe zenyewe binafsi.

“Kwa sasa tunatakwia kuimarisha sekta hizi binafsi kwa kuzipatia
misaada na sera ili ziweze kutekeleza majukumu yake katika kukuza
uchumi,” alisema Makamu huyo wa Rais. Kwa upande wake Waziri wa Fedha a Uchumi, Mustafa Mkullo akizungumzia suala la ukosefu wa ajira wka vijana alisema kwua kutokana ana asilimia 53.5 ya watanzania wote nchini kwua vijana ambao wana umri kati ya mika 15-35 ambapo kati ya asilimia 68 kati yao hawana ajira.

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kulia) akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilali(kushoto) jana mjini Arusha katika Hotel ya Mount Meru kwa ajili ya kufungua mkutano wa 20 wa Bodi ya Magavana unaofanyika Tanzania (Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO-Arusha)


Alisema kutokana na hilo serikali imeweka mikakati madhubuti ikiwa ni
pamoja na kuboresha vyuo vya ufundi ili viweze kutoa mafunzo yatakayo wezesha vijana kuwea kujiajiri wenyewe. Mkullo alivitaka vyuo vikuu na vile vinavyotoa elimu ya juu kutoa mafunzo yatakayowawezesha vijana kuweza kujiajiri wenyewe.