Mahakama Nchini Brazil Yamkaba Neymar

neymar

Mahakama moja ya Brazil imepiga tanji mali ya mchezaji nyota wa Barcelona, Neymar.

Mahakama hiyo iliopo Sao Paulo ilitangaza kuwa inatoa waranti ya kuzuia mali yenye thamani ya takriban dola milioni 50 ya mchezaji huyo wa Brazil.

Mali hiyo inashirikisha ndege,jahazi la kifahari na Mali nyengine.Neymar mwenye umri wa miaka 23 ametuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi kati ya mwaka 2011 na 2013 na anakabiliwa namshataka ya kujibu.

Miongoni mwa mali zilizozuiwa ni kampuni tatu zinazomilikiwa na familia yake.Waendesha mashtaka wanamtuhumu Neymar kwa kuanzisha kampuni ambazo zilimsaidia kulipa kiwango kidogo cha ushuru.

Wanataka alipe dola milioni 16 kama kodi ambayo haikutangazwa. Mahakam hiyo iliagiza mali yake kupigwa tanji ili kuhakikisha kuwa anafanya malipo hayo pamoja na faini.

Hatahivyo Neymar anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama na kwamba sio rahisi kwa yeye kuhudumia kifungo,kulingana na mkaguzi mmoja wa maswala ya fedha.