Serikali Yaahidi Kumsaidia Mwanahabari Athumani Hamisi

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa na mwanahabari Athumani Hamisi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwa na mwanahabari Athumani Hamisi.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisalimiana na Athumani Hamisi alipomtembelea nyumbani kwake Sinza Madukani jijini Dar es Salaam.Athumani Hamisi alikuwa Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habari Leo, yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper, ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake kutokufanya kazi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza waandishi wa habari ambapo alisema Serikali itaendelea kumsaidia Athumani Hamisi na kutafuta suluhisho la kudumu. Athumani Hamisi alikuwa Mpigapicha Mkuu wa Magazeti ya Daily/Sunday News na Habari Leo, yanayomilikiwa na Serikali kupitia Shirika lake la Standard Newspaper, ambaye alipata ajali iliyomsababishia baadhi ya viungo vyake kutokufanyakazi

Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na michezo Nape Nauye ameahidi kutatua changamoto zinazomkabili aliyekuwa mpiga Picha na mwandishi mwandamizi Athumani Hamis. Wazir Nape ametoa kauli hiyo alipomtembelea nyumbani kwake, Sinza Dar es salaam akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Global Publisher Eric Shigongo.

Waziri Nape ameamua kumtembelea Athmani kutokana na kutambua mchango wake kwenye tasnia ya habari ambapo aliitumikia kwa muda mrefu kabla ya kupata ulemavu. “Amefanya Kazi kubwa serikalini, sisi kama serikali tunao wajibu wa kumsaidia”. “Nimechukua Yale yote ambayo yanachangamoto kwake na tunachukua uamuzi wa kumsaidia,”alisema Wazir Nape.

Waziri Nape amempongeza Rais MstaafuJakaya Kikwete kwa kumsaidia Athmani katika kipindi chote cha uongozi wake na kwamba yeye kama Waziri mwenye dhamana kwa kushirikiana na wadau wengine wataendelea kutoa msaada kwa Athmani na familia yake.

Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ndugu Eric Shigongo ametoa wito kwa Watanzania kutoa msaada kwa moyo mmoja.