Utamu wa UEFA Umerejea, Chealsea Kuivaa PSG

140828174348_sorteio_uefa_champions_league_getty_624x351_getty

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya (Uefa champion Ligi) itaendelea tena siku ya Kesho Jumanne Usiku kwa Mechi 2 za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16.

Benfica ya ya Ureno itakuwa nyumbani dhidi ya Zenit Saint Petersburg na Paris St Germaine itakuwa Nyumbani Jijini Paris ufaransa kuwavaa Mabingwa wa England Chelsea.

PSG

Na Jumatano, zitapigwa mechi ambapo Klabu ya KAA Gent ya ubelgiji watakuwa Nyumbani kucheza na Wajerumani VfL Wolfsburg ,huku AS Roma ya Italy wakiwa nyumbani kupambana na Vigogo wa Spain Real Madrid.