Na Frank Shija, WHUSM
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya Kilimanjaro Marathoni yatakayofanyika tarehe 28 Februari kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi. Hayo yamebainisha na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Executive Solution ambayo ndio waratibu wa mbio hizo Bw. Aggrey Marealle walipotembelea ofisini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.
“Mbio za Kili Marathon zinatarajia kufanyika tarehe 28 mwezi huu katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ambapo mgeni rasmi atakuwa Mhe. Nape Moses Nnauye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo”. Alisema Marealle.
Marealle alisemakuwa Mbio hizo zitakuwa katika makundi manne ambayo ni mbio za Kilomita 42 ambazo ndiyo marathoni yenyewe inayothaminiwa na TBL kupitia bia ya Kilimanjaro,zingine ni Nusu Marathon za kilomita 21 zinazodhaminiwa na Tigo,mbio za kilomita 10 zinazowashirikisha walemavu wanaotumia Baiskeli za matairi matatu na Viti vya matairi zinazodhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Gapco na mbio zinginge ni za kilomita 5 ambazo zinadhaminiwa na TBL kupitia kinywajji cha Grand Malt.
Aliongeza katika mbio hizo washindi kumi kila kundi watapewa zawadi ambapo mshindi wa kwanza kwa mwanaume na mwanamke katika mbio za kilomita 42 watapatiwa zawadi ya shilingi milioni nne kila mmoja.
Aidha alisema kuwa zaidi ya washiriki 7000 wanakadiriwa kushiriki mbio hizo huku kati yao takribani washiriki 1000 watatoka nje ya nchi.
Kilimanjaro Marathon inatimiza miaka 14 tokea kuanzishwa kwake ambapo waandaji wa mashindano hayo ni Kampuni ya Wild Frontiers ya Afrika Kusini na kuratibiwa na Executive Solutions Ltd ya Tanzania na mdhamini mkuu wa mbio hizo ni Kampuni ya Bia TBL kupitia Bia ya Kilimanjaro Lager.