Barabara za Mzunguko Kuanza Kujengwa Dar Juni

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (wa tatu kulia), huku Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama akifatatilia maelezo hayo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akifafanua hatua za Serikali za kuhakikisha ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam unakamilika mwezi juni mwaka huu.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akifafanua hatua za Serikali za kuhakikisha ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam unakamilika mwezi juni mwaka huu.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa barabara za mzunguko (ring roads) zenye lengo la kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam utakamilika baadae Mwezi Juni mwaka huu.
Amesema kufuatia Serikali kuanza kulipa madeni ya makandarasi amewataka makandarasi wote kurudi kazini ili kufikia lengo la Serikali la kukamilisha barabara hizo mwezi juni sambamba na ulipaji wa madeni yote.
“Tunawaomba wale wenye nyumba pembeni mwa barabara za mzunguko ambao wapo kwenye orodha ya kulipwa fidia waondoke maeneo hayo ili kuruhusu kazi ya ujenzi wa barabara kuendelea”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amekagua barabara za Tankibovu – Goba (km9), Goba – Mbezi Mwisho (Km7), Kimara Baruti – Msewe – Chuo Kikuu (km2.6), Mbezi Mwisho – Malambamawili – Kifuru – Kinyerezi (km14), na Tabata Dampo – Kigogo (km1.6).
Barabara hizo zenye urefu wa Km 27.2 zimejengwa kwa gharama ya takriban sh. bilioni 56.3 ikiwa ni gharama za ujenzi na fidia ambazo zote zinalipwa na fedha za mfuko wa barabara.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale amewataka madereva kulinda barabara hizo kwa kutoegesha magari katika maeneo yasiyoruhusiwa na kukemea vitendo vya uchimbaji mchanga pembeni mwa madaraja.
Waziri Prof. Mbarawa pia amekagua ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40 lililojengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 2.3 ambao ujenzi wake umekamilika.
Barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam zinajengwa kwa kiwango cha lami ili kuvutia magari mengi kutumia barabara hizo na kupunguza msongamano katikati ya jiji ambapo hadi sasa Km 27 zimekamilika na Km 28 zinaedelea kujengwa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.