Mke Wa Waziri Mkuu Anusurika Kufa Kwenye Ajali

Gari STK 9442 alilokua akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda likiwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali hii jana jioni eneo la Mkundi mkoani Morogoro.

Mke wa waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda amenusurika kifo baada ya gari alilokua akisafiria kugongana na pikipiki mkoani Morogoro jana jioni.

Mama Pinda aliyekua akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam akitumia gari STK 9442 liligongana na pikipiki MC647 BBA na kupondika eneo la Mkundi mkoani Morogoro majira ya saa 8 mchana hiyo jana.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kua chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa bodaboda aliyeingia barabarani bila tahadhari na kupelekea mama Pinda, msaidizi wake na dereva kupata majeraha huku mwemda bodaboda huyo akipoteza maisha.

pida

Majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro ambapo walipatiwa matibabu kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutenge ni miongoni mwa viongozi waliofika eneo la tukio na kuwatembelea majeruhi katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.