CCM Yateuwa Wagombea Uenyeviti Mikoa, U-NEC…!

Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimewataja wagombea nafasi za uwenyeviti wa CCM mikoa iliyoachwa wqazi pamoja na wagombea wa nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho taifa, NEC nafasi ambazo hadi sasa zilikuwa wazi baada ya viongozi waliokuwepo kupoteza maisha kwa baadhi na wengine kukihama chama na kujiunga na UKAWA.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa iliyokutana Mjini Dodoma katika kikao maalumu imepitisha majina ya wagombea wa nafasi hizo baada ya kupembua majina ya waliojitokeza.

Alisema kwa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Arusha imempitisha Michael Lekule Laizer, Emanuel Makongoro Lusenga na John Pallangyo kugombea nafasi hiyo, huku kwa Mkoa wa Shinyanga imewapitisha Hassan Ramadhani Mwendapole, Mbala Kashinje Mlolwa na Erasto Izengo Kwilasa kugombea nafasi hiyo iliyowazi kwa sasa.

Nnauye alisema kwa nafasi ya uwenyekiti Mkoa wa Singida kikao hicho kimewapitisha Hanje Narumba Barnabas, Misanga Mohamed Hamis, Mlata Martha Moses pamoja na Kilimba Juma Hassan watakaochuwana katika nafasi hiyo. Aliwataja wateuliwa wengine wa nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, NEC kwa Nyamagana kuwa ni Dk. Sillinus Elias Nyanda, Jamal Abdul Babu, Kelebe Bandoma Lutelil na Patrick Kambarage Nyabugongwe.

Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Na kwa Kahama waliopitishwa ni Pili Yakanuka Izengo, Paschal Ndibatyo Mayengo pamoja na Sweetbert Charles Nkuba; huku kwa Monduli amepitishwa mgombea mmoja Namelock Edward Sokoine. Wagombea wengine waliopitishwa kugombea nafasi za uenyeviti wa CCM Wilaya ni pamoja na Loata Erasto Sanare (Monduli), Chami Slegried Mask na Godfrey Mwimanzi Mwikala (Sumbawanga Mjini). Kikao hicho pia kilipitisha wagombea nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Arusha na wagombea uenyeviti wa UVCCM mikoa ya Arusha na Sinyanga.

Katika hatua nyingine kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Jakaya Kikwete (rais mstaafu wa Tanzania) kilipokea taarifa ya maandalizi ya marudio ya uchaguzi wa Zanzibar, na kuridhishwa na mchakato wa maandalizi ndani ya CCM hivyo kuwatakia kila la heri Wazanzibari katika uchaguzi huo. Pia Kamati kuu imetoa pole kwa Jeshi la Polisi kwa kuondokewa na askari wake watatu mkoani Singida mara baada ya kupata ajali wakitekeleza majukumu yao.