AGIZO la Serikali kuzuia usafiri wa bodaboda mjini umegeuka kuwa kitega uchumi kwa baadhi ya vijana walioajiriwa kuhakikisha agizo linatekelezwa. Hii imethibitika baada ya mwandishi wa habari hizi kufumania tukio la vijana wa jiji wakidai rushwa wazi wazi bila woga kwa mwendesha pikipiki wa magurudumu watatu maarufu kama bajaji.
Kachero wetu (jina limehifadhiwa) alifanikiwa kupata picha za wala rushwa pamoja na kunasa sauti za tukio lote.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tambaza wakiwa pembezoni ya barabara katika daraja la Salenda.
Mmoja wa mfanyakazi wa Tambaza akisimamisha bajaji.
Wafanyakazi wa Tambaza (walio na mashati ya rangi nyeupe) wakizungumza na dereva wa bajaji.
Chanzo Mo Blog