Kipute Ligi Kuu ya Uingereza Kuendelea tena Leo

160123145537_liverpool_norwich_640x360_getty_nocredit

Ligi kuu ya England inatarajia kuendelea tena leo jumanne kufuatia mapumziko ya michuano ya FA, kwa michezo kadhaa,ambapo Arsenal watawakaribisha Southampton,Leicester city watakuwa wenyeji wa Liverpool, Norwich watakuwa wakimenyana na Tottenham Hotspurs.

Michezo mingine Sunderland watawaalika Manchester City, Aston Villa watakuwa wageni wa West Ham United,Crystal Palace watawakaribisha Bournemouth, Stoke watakuwa wenyeji wa Manchester Unted na West Brom watachuana na Swansea city.

Mpaka sasa Leicester city wanaongoza ligi kwa alama 47 ikifuatiwa na Manchester city katika nafasi ya pili,nafasi ya tatu ni Arsenal na nafasi ya nne ni Tottenham.