Rwanda Watupwa Nje na Congo Michuano ya CHAN

chan

Timu ya Congo imefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya CHAN baada ya kupata goli lake kunako dakika ya 11 kupitia mchezaji wa kiungo Doxa Gikanji aliyekunjua shuti kutoka mita 18.

Wachezaji wa Rwanda hawakutarajia goli hilo na wameonekana kukatishwa tamaa na goli hilo la mapema mbele ya mashabiki wao zaidi ya elfu 20 waliojazana kwenye uwanja wa taifa Amahoro.

Congo ilitawala kipindi cha kwanza kwa chenga,pasi na mbwembwe za kila aina. Kipindi cha pili mambo yalibadilika

Dakika ya 24 nusura Congo wapate goli la pili.Mpira uliopigwa ghafla na mshambuliaji Elia Meschack ulirudishwa na mlingoti wa lango.

Nafasi pekee ya kutishia lango la Congo ilikuja kwenye dakika ya 37 mpira uliopigwa na mshambuliaji Jacques Tuyisenge ulilazimisha kipa wa Congo kufanya kazi ya ziada kuokoa jahazi lake.

Katika kipindi cha pili Rwanda ilikuja juu na kutawala mchezo hadi dakika ya 57 ilipoandikisha goli la kusawazisha kupitia mshambuliaji Ernest Sugira.

Hadi dakika 90 kumalizika matokeo yameendelea kuwa hayo.Goli la ushindi la Congo lilipatikana kwenye dakika ya 114 kupitia mchezaji Botuli Bompunga,aliyiwezesha Congo kutinga nusu fainali.