Tanzania kuadhimisha siku ya Ukoma Duniani

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani

 Mratibu wa Ukoma toka  Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani

Mratibu wa Ukoma toka Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani

Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

Tanzania inaungana na nchi nyingine Duniani itaazimisha siku ya Ukoma Duniani itakayoadhimishwa tarehe 29 Januari 2016 kwa kutoa elimu juu ya kujikinga na kupambana na ukoma Tanzania na kuifanya Tanzania iweze kuondokana na maambukizi mapya ya ukoma.

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ikiwa ni harakati za serikali kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa elimu kwa umma wa watanzania.

Mhe.Ummy Mwalimu amesema siku hii itawapa fura ya kutathimini mwelekeo wa jitihada za nchi na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu ambao umekuwa ukiogopwa sana katika jamii yetu toka enzi na enzi hasa kutokana na ukweli kwamba unasababisha ulemavu wa kuduma.

“Kwa mujibu wa takwimuza mwaka 2014,jumla ya wagonjwa 2,134 wa ukoma waligunduliwa ambapo wagonjwa 271 kati ya hao ambao ni sawa na asilimia 13walikuwa na ulemavu na pia bado kuna Wilaya 17 za Tanzania bara na 2 za Tanzania Visiwani zilizogunduliwa idadi kubwa ya wagonjwa wa ukoma”

“ Nizitaje wilaya hizi ambazo zimekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa ukoma kwa Tanzania bara ni Liwale,Ruangwa,Lindi Mjini,Lindi Vijini,Masasi Vijijini,Newala,Nanyumbu,Namtumbo,Tunduru,na Nkasi. Nyingine ni Mkinga,Muheza,Korogwe,Musoma,Korogwe,Musoma Vijijini ,Chato,Shinyanga Manispaa na Rufiji na kwa Tanzania Visiwani ni Mkoa wa Mjini Magharibi na katika wilaya za kati na kusini. Alisema Mhe Mwalimu

Aidha amesema kuwa Tanzania katika kuadhimisha siku hii Serikali inayashukuru mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa michango yao katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukoma hapa Tanzania na hivyo kuhakikisha tunakuwa na Tanzania isiyo na maambukizi mapya ya ukoma.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 17 Duniani ambazo bado zina viwango vya juu vya ugonjwa wa ukoma na kwa zaidi ya miaka 62, siku ya ukoma Duniani imekuwa ikiadhimishwa ulimwenguni kote kila Jumapili ya mwisho wa mwezi wa Januari.