Breaking News: Samatta Asaini KRC Genk Mkataba wa Miaka Mitano

1

NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta tayari ametambulishwa rasmi na ameshakabidhiwa jezi na klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuanza majumu mapya ya kutupia wavuni akiwa na klabu hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu ya Genk, Samatta amesaini mkataba unaomalizika msimu wa mwaka 2019-2020.

Samatta amejiunga na Genk akitokea TP Mazembe ambapo alicheza kwa miaka mitano (5) tangu mwaka 2011 alipojiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Simba SC hadi mwaka 2015.

3

Mkataba wa Samatta na Mazembe ulikuwa unamalizika mwezi April mwaka huu lakini tayari amesaini mkaba mpya na klabu hiyo ya barani Ulaya.
Samatta amesema hataki matatizo na klabu yake ya zamani, TP Mazembe na anaomba wafikie mwafaka na klabu yake mpya, KRC Genk.

Samatta ameyasema hayo leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo mjini Genk wakati wa kutambulishwa kwake kujiunga na klabu ya Koninklijke Racing Club Genk kwa Mkataba wa miaka mitano.

4

Samatta amesema Mazembe ilimchukua akiwa kijana mdogo na anaishukuru kwa kumlea vizuri na kukuza kipaji chake hadi kutimiza ndoto ya kucheza Ulaya

Samatta aliyezaliwa Desemba 23, mwaka 1992, anaondoka Mazembe baada ya kushinda nayo taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, ubingwa wa Ligi Kuu ya DRC mara nne na Super Cup ya DRC mara mbili.

Aliyejiunga na Mazembe ya Lubumbashi, DRC mwaka 2011 akitokea Simba SC aliyoichezea kwa nusu msimu baada ya kujiunga nayo kutoka African Lyon, zamani Mbagala Market, Mkataba wake na KRC Genk unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2020.
Chanzo cha habari na www.shaffihdauda.co.tz