Hii Tarehe Mwigizaji Lulu Hawezi isahau Maishani Mwake

LUL

Katika maisha ya kila mwanadamu anasiku maalum ambayo hawezi kuisahau iwe ni kumbukumbu kwa jambo zuri au baya, ila bado mtu atakuwa anaikumbuka.

Tarehe kama ya leo ya tarehe 28 mwezi wa kwanza mwaka 2013, ni siku ambayo mwigizaji wa Kitanzania Lulu Michael hataweza kuisahau katika maisha yake, ambapo ilikuwa siku ambayo alipata dhamana katika mahakama Kuu ya Kisitu jijini Dar es Salaam baada ya kukabiliwa na Kesi ya kusababisha Kifo cha Mwigizaji mwezake Stivi Knumba.

8STV KANU

LULU

Stivin Kanumba alifariki tarehe ya saba mwezi wa nne mwaka 2012 akiwa nyumbani kwake pamoja na Lulu.

Mwigizaji Lulu alipewa dhamani baada ya kukamilisha masharti manne aliyopewa na mahakama, ambayo ni:
(i) Kuacha hati yake ya kusafiria Mahakamani.
(ii) Kutokusafiri Nje ya jiji la Dar es salaam bila kibali cha Mahakamani.
(iii) Kuripoti mahakamani kila tarehe moja ya mwezi
(iv) Kuwa na wafadhiri wenye Bondi ya shilingi milioni 20
Na hatimaye tarehe 29 mwezi wa kwanza alipewa dhamana na kuruhusiwa.